Advertise here

Saturday, January 26, 2013

OMMY DIMPOZ NA VANESSA MDEE KUANZA KUSHOOT ME & U

Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee wakisindikizwa na AY, jana wamewasili salama jijini Nairobi Kenya ambako wameenda kushoot video ya Me and You.
 
Video hiyo inafanywa na kampuni ya Ogopa Dj’s ambayo hivi karibuni ilishoot video ya Diamond, Kesho. Me and You ni single ya tatu ya Ommy yenye mafanikio makubwa.

MSANII MATUMAINI YU MAUTUTI MSUMBIJI

MCHEKESHAJI maarufu Bongo Aliyewahi kutamba na kundi la kaole, Tumaini Martin Mwakibibi ‘Matumaini’ anadaiwa yu mahututi nchini Msumbiji ambako alikwenda kwa ajili ya kufanya shoo akiwa na mchekeshaji mwenzake, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’.
 
Akizungumza na na safu hii leo jijini Dar, Herieth Chumila ambaye pia ni msanii, alisema alipokea taarifa za kuumwa kwa Matumaini kutoka kwa mtoto wake aishiye nchini humo na kumwomba msaada wa haraka kwa kuwa msanii huyo yupo katika hali mbaya.
Herieth alisema kwa sasa msanii huyo hawezi hata kutembea na mahitaji muhimu ya kibinadamu anayamalizia kitandani.
 
 “Nilipata bahati ya kuongea na Matumaini ingawa kwa shida sana, aliwaomba Watanzania tumsaidie ili arudi nyumbani. Alisema ni bora aje kufia huku kuliko nchi za watu,” alisema Herieth.
 
Akaongeza: “Kwa yule ambaye ataguswa kumchangia awasiliane na mimi kwa ajili ya mchango ambao utamfikia Matumaini kule Msumbiji.”

MSANII WA BONGO MATATANI KWA VAA VIATU VYENYE SIRAHA


MTANGAZAJI wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida,’ hivi karibuni alinaswa akiwa amevalia kiatu ambacho kina silaha.

Kiatu hicho ambacho ni moja ya fasheni zilizoingia, kina misumari pembeni kiasi kwamba akikurushia teke, ni lazima kikutoboe.
Baadhi ya watu waliokiona kiatu hicho walisema kuwa, licha ya kwamba ni fasheni lakini atakayekivaa lazima watu wamgwaye.
“Sasa hiki ni kiatu au silaha? Ukikivaa kwenye msongamano wa watu si utajeruhi, mh! Hizi fasheni za sasa mbona balaa,” alisema Zuhura wa Kinondoni.

MOVIE MPYA YA DOKTA CHENI COMING SOON...


65879_522522841113760_872229244_n

DOWNLOAD UJIO MPYA WA NOORAH _ALI KIBA _NIKUP_ NINI