Advertise here

Wednesday, January 30, 2013

WAKATI G.UNIT HAWANA MKWANJA MAMBO YALIKUWA AAH FRESH!!

Kwa muda kumekuwa na stories kibao tofauti tofauti zisizo nzuri kuhusiana na G.Unit Crew, 50 cent mwenyewe amekubali washkaji kweli hawaongei kama vile kwa sasa. Akipiga stories na MTV Tony Yayo alizungumza juu ya hilo. Alisema kipindi wakiwa na mkwanja mambo yalikuwa mabaya sana mkwanja ndo chanzo cha ushetani wote, lakini kipindi tukiwa hatuna mkwanja mambo yalikuwa fresh tu, Alisema hivyo akipiga stories na MTV.

CHRISS BROWN NDANI YA DRAMA NYINGINE

Siku nyingine tena, Drama nyingine tena, lakini sio msanii mwingine, msanii ni Yule Yule mkali ambae anadrama kibao, juzi wakaleteana noma na Frank Ocean. Sasa basi unakumbuka siku za nyuma Chriss Brown alidelete twitter account yake? na baada ya siku mbili au moja baadae akairudisha ilikuwa ni baada ya kujibishana sana na mtu kwenye twitter.  Drama za Chriss Brown muda mwingine huwa zinasababishwa na yeye mwenyewe au saa nyingine unakuta hausiki. Sasa basi Mshikaji Chriss Brown kufuatia drama yake na Frank Ocean juzi kati ameamua kufuta instagram yake na alikuwa akiandika meseji za drama ile mbaya na kutangaza kuondoka kwake yani kufuta instagram yake, Swali ni kwamba, Je Chriss Brown atarudi tena instagram kama alivyofanya kwenye twitter au ndo ntoleeeee? Turn Up Lol!