Advertise here

Monday, February 04, 2013

XAVI HERNÁNDEZ NJE KWA SIKU 15

Baada ya kufanyiwa majaribio asubuhi ya leo Xavi Hernandez imegundulika kwamba atakuwa nje kwa takribani siku 15 na atakosa mechi mbili zijazo kati ya Getafe na Granada, Ingawa kupona kwake kunaenda kama ilivyopangwa, Xavi atarudi uwanjani wakati michezo ya Champion League wakicheza na Milan mechi itakayochezwa tarehe 20 mwezi 20. Xavi pia atakosa pia mechi kati ya kirafiki dhidi ya Uruguay Jumatano. Xavi amecheza mara 33 msimu huu na amefunga magoli 6, Xavi alicheza karibia mechi yote Jumapili pale Mestalla na alitoka na kubadilishana na Thiago katika muda wa nyongeza.

MADUKA YATEKETEA KWA MOTO MWENGE

Hivi ndivyo eneo la Mwenge kituoni lilivyokuwa majira ya saa tano asubuhi ambapo shughuli zote ikiwemo usafiri wa Daladala kuelekea katikati ya Jiji na maeneo mengine zilisimama ili kupisha vikosi vya Zima Moto na Uokoaji vya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuzima moto uliokuwa ukiteketeza baadhi ya maduka.
Licha ya Moto huo kuonesha kuwa na madhara zaidi, vikosi vya zimamoto vikishirikiana na vile vya Kampuni binafsi za Ulinzi vilifanikiwa kuuzima moto huo na kupunguza hatari ya kuhamia kwenye maduka mengine ambayo yamekaribiana.
Akizungumzia tukio, Mkuu wa Ulinzi Shirikishi Kituo cha Mabasi Mwenge KESSY MLUGURU amesema, waligundua kutokea kwa moto huo katika moja ya duka majira ya saa tatu asubuhi na kuanza juhudi za kuuzima kwa maji yakiyo kwenye tenki ambapo Mkuu wa Kituo cha Polisi Mabatini Kijitonyama anathibitisha kutokea kwa moto huo.
Mmoja ya Wamiliki wa maduka ya vipodozi ambayo yameteketea MAPINDUZI WILSON amesema, moto huo umetokea kutokana na hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye moja ya waya zinazoingia kwenye maduka hayo.
Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, Meja KURWA NZELEKELA amesema kikosi chake kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu ya barabarani na usalama wanapokuwa kazini.
Tukio hili linafuatiwa na lile lililotokea jana kwenye Jengo la PPF TOWER lililopo Makutano ya Mtaa wa Ohio na Garden kunusurika kuteketea kwa moto baada ya moja ya ghorofa zake kushika moto ambao pia ulidhibitiwa na vikosi hivyo vya zima moto.

TUME YA KUKUSANYA NA KURATIBU MAONI YA KATIBA YAMALIZA HATUA ZA MSINGI

Tume ya kukusanya na kuratibu Maoni ya Katiba nchini imesema imemaliza hatua ya msingi ya kukusanya na kuratibu maoni kutoka kwa makundi maalum na kubainisha kuwa hatua inayofuata sasa ni kuanza kwa zoezi la uchambuzi wa maoni yote yaliyokusanywa pamoja na uandishi wa rasimu ya katiba mpya.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu JOSEPH WARIOBA amesema kuwa uchambuzi huo unatarajiwa kufanywa na mabaraza maalum ya Katiba kuanzia June Mwaka huu, na kuongeza kuwa mabaraza hayo yatapatikana kupitia mapendekezo maalum kutoka kwa wajumbe wa Tume hiyo.
Akizungumzia uteuzi wa mabaraza hayo JAJI WAROBA amesema, tume hiyo imejipanga kuhakikisha watu watakaopatikana kuunda mabaraza hayo wanakuwa makini, na ambao watasimamia zoezi hilo haraka na kwa umakini zaidi ili kupata katiba itakayokuwa na tija kwa Watanzania.

LEO KATIKA ITV HABARI


  • Jeshi la polisi kikosi cha zimamoto limepanga kufungua vituo saba katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam ili kukabiliana na tatizo la msongamano ya magari linalosababisha kuchelewa katika matukio ya moto yanayoanza kujitokeza kwa kasi kubwa hapa nchni.
    21 minutes ago
  • Kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini TFF imemuondoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa chama hicho Michael Wambura aliyekuwa akiwania nafasi ya umakamu wa rais.
    23 minutes ago
  • Moto uliozuka katika maduka ya eneo la Mwenge kituo cha mabasi umedhibitiwa na vikosi vya zimamoto na sasa hali ni shwari ingawa shughuli nyingi za kibiashara bado zimesimama wahusika wakihofia usalama wa mali zao.

BRAND NEW TACK C-SIE MADIN_ft_JOSEFLY_NDANGU

Download New Audio Song | KIGOMA ALL STARS `NYUMBANI'