Advertise here

Wednesday, March 13, 2013

VIDEO MPYA YA ALICIA KEYS YAZUA BALAA


Video ambayo Alicia Keys ameiachia mtandaoni kama utambulisho wa Uzinduzi rasmi wa Video yake mpya ambayo jina lake tayari limekwishaanza kuzua gumzo kubwa kila kona... Bibie huyu ameamua kuipatia video yake mpya jina "Illuminate Me".... Issue ambayo inawafanya wengi wa mashabiki zake kuzidi kumhusisha na 'Illuminati' (Jamii ya siri inayoaminika kuwa ni ya Kishetani).




#JFYI Video hii ni sehemu ya mchongo wa Alicia na kampuni ya BlackBerry kwaajili ya ziara yake ya 'Set The World On Fire' huko Los Angeles Marekani ambayo wao wanaitumia kutangaza toleo lao la simu - #BlackBerry10 

Wadau wote kwa sasa wanasubiria kuona ni nini Alicia Keys atakachokifanya ndani ya 'Illuminate Me' ...so do you!!. 
Picha ya Alicia backstage masaa machache kabla ya kupanda jukwaani leo huko Los Angeles

harusi ya 2 face Idibia & Annie Maculay's

 Mwanamuziki Kutoka Nigeria ambaye alitamba na nyimbo ya 
My African Queen,Ole na nyinginezo ameachana na ukapela na kumpata Queen wake




























JUSTIN BIEBER CHUKUA MAAMUZI KABLA HUJAPOTEZA WASHABIKI A SELENA: BONNIE

Justin Bieber Bad Boy
Justin, I know breakups are hard and that you’re under tremendous work pressure, but you need to stop acting out in frustration! There are too many people who depend on you and consider you a role model. It’s time to start behaving like the great guy we all know you can be and put an end to all this craziness! Justin Bieber – I understand that it hasn’t been easy getting over your longtime girlfriend Selena Gomez. You’ve worked incredibly hard to try and win her back, but she’s hardly even taking your phone calls anymore. That must really hurt.

And it never feels good to see an ex thriving after he or she leaves you, so watching Selena revenge dress during her Spring Breakers promotion tour must really feel like she’s twisting the knife. Plus, you’re in the midst of a 124 date , almost year-long world tour and you’re probably exhausted already. No wonder you were having trouble breathing during one of your shows in London. Maybe you’re so stressed out, you were actually having an anxiety attack on stage. Hey, most of us would have an anxiety attack if we had to go around the world and perform 124 shows — talk about the jet lag alone!

WAJITOKEZA KUISAIDIA POLISI KIFO CHA PADRE ZANZIBAR

Zanzibar. Polisi imeanza kupokea majina ya watu wanaodaiwa kumuua Padri Evarist Mushi kutoka kwa wananchi, kutokana na mchoro uliotolewa unaoonyesha sura ya mtu anayedaiwa kumuua padri huyo.
Wananchi wamepiga simu polisi au kwenda kutoa majina ya watu wanaodhani wamefanana na mchoro wenye taswira ya mtu anayedaiwa kumuua Padri Mushi.
“Wametupigia simu na wengine wamekuja, kutwambia mtazameni fulani au fulani na sisi tunachunguza watu hao tuliotajiwa,” alisema Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa.
Kamishna Mussa alisema mchoro huo umetolewa na Polisi Tanzania  wala siyo Askari wa Upelelezi wa Marekani (FBI), ambao wapo kusaidia kumsaka muuaji.
Kuhusu mchoro huo kumwonyesha mtu aliyevaa baraghashia, alisema kwa Zanzibar hilo ni vazi la utamaduni wala siyo la dini na  kwamba, anaweza kuwa alikuwa mtu kutoka Bara lakini alivaa hivyo ili kupoteza kufahamika.
Alisema uchunguzi mkali unaendelea, lakini hadi sasa hawajamnasa mtu ambaye wana ushahidi wa kutosha kumpeleka mahakamani.
Polisi juzi walitoa mchoro unaomwonyesha mtu anayedaiwa kumpiga risasi na kumuua Padri Mushi wa Kanisa Katoliki, Februari 17 mwaka huu.

Dk Slaa amkumbuka Sitta


Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa akizungumza  na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana. Kulia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. Picha na Rafael Lubava                            


Posted  Jumanne,Marchi12  2013  saa 20:36 PM
Kwa ufupi
Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu wabunge wa chama hicho kutakiwa kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema Spika Makinda amekuwa akipindisha kanuni na ndiyo maana kumekuwa hakuna utulivu bungeni.
 
Mvutano uliopo hivi sasa kati ya Chadema na Bunge ulianza Februari 4 katika kikao cha Bunge mjini Dodoma baada ya wabunge wa Chadema kupinga msimamo wa kiti cha Spika wakieleza unapendelea


Boniface Meena na Mussa Juma, Mwananchi
Kutokana na mvutano ambao umekuwapo mara kwa mara kati ya Chadema na Spika wa Bunge, Anne Makinda, chama hicho kimemkumbuka aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Samuel Sitta kikieleza kuwa alikuwa hapindishi sheria na kanuni za Bunge na ndiyo maana lilikuwa limetulia.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu wabunge wa chama hicho kutakiwa kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema Spika Makinda amekuwa akipindisha kanuni na ndiyo maana kumekuwa hakuna utulivu bungeni.

“Spika Sitta aliyekuwepo kabla ya Makinda alikuwa hapindishi sheria na alikuwa anajirekebisha pale anapokosea na tulikuwa tukishauriana kwamba asijihusishe na mambo ya vyama,” alisema Dk Slaa.

Alisema Sitta, ambaye hivi sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alikuwa hafuati mambo ya vyama kwa kuwa alitakiwa kuwa ni mtu ambaye hapendelei upande wowote. Sitta, ambaye alikuwa Spika kuanzia mwaka 2005-2010, alikuwa anajinadi kwa kuendesha Bunge kwa spidi na viwango.

“Makinda aachane na ushabiki wa CCM kwani anajua kabisa kanuni ya nane inamtaka Spika asifungamane na upande wowote hivyo aache kufanya hivyo,” alisema Dk Slaa.

Alisema ni muhimu Spika akawaeleza kimaandishi amepata wapi mamlaka ya kuruhusu kamati iendelee wakati zote zilivunjika rasmi katika Bunge lililopita.
“Spika kama hajui kanuni aende shule kujifunza kuliko kututia aibu, wanasheria, wabunge wamsaidie ili aweze kuelewa.”

Dk Slaa alisema katika mabunge ya kidemokrasia, kupongeza ni jambo halali na kuzomea pia ni jambo halali hivyo kitendo cha wabunge wao kuzomea ni sawa kwa kuwa ni njia yao ya kufikisha ujumbe. Akizungumzia suala la wabunge wake kuhojiwa na kamati hiyo ya Bunge, alisema hawatakwenda kuhojiwa na kamati hiyo na kama Bunge litaamua kuwafukuza lifanye hivyo ili wananchi waelewe.

“Hawawezi kwenda kuhojiwa na kamati ambayo haipo kisheria, nilipokuwepo bungeni nilishiriki kuandaa kanuni hizi za Bunge, Spika hana mamlaka anayojipa ya kuongeza muda wa kamati, hivyo aache kulidhoofisha Bunge na badala yake alisaidie,” alisema Dk Slaa.

Akizungumzia suala hilo, Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema anashangazwa na Naibu Spika, Job Ndugai kusema kuwa kuna kamati ambazo huwa zinaendelea wakati nyingine zinapokuwa zimemaliza muda wake.

Lema aitisha maandamano
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, ametangaza kuandaa maandamano makubwa yatakayoshirikisha wanawake na watoto katika Jiji la Arusha ili kushinikiza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA) kuwasambazia maji.

Akizungumza jana, Lema alisema ameamua kuandaa maandamano hayo ya kudai maji kwani kwa zaidi ya miezi sita sasa asilimia 70 ya wakazi wa Jiji la Arusha hawapati maji safi.

“Nimewaandikia barua AUWSA wiki mbili sasa nikiwataka wanipe mipango yao ya muda mfupi na mrefu ya kuondoa tatizo la maji Arusha, kwani mimi kama mbunge ninaweza kushirikiana nao kupunguza tatizo hili, lakini hawajajibu sasa tutawashinikiza kwa nguvu wa umma,” alisema Lema.

kipanya MARCH