Advertise here

Friday, April 12, 2013

cheki Jaden Smith -THE COOLEST (Official Video) HD

cheki AcE ft. Jaden & Willow Smith - Find You Somewhere

After Earth Official Trailer #2 (2013) - Will Smith Movie HD

CAMP MULLA WATETE BAADA YA KUTENGANA


Uvumi umezidi kutanda kuhusu kutengana kwa wasanii wanaoliwakilisha kundi maarufu la Camp Mulla la nchini Kenya na ukweli wa jambo hilo limewekwa wazi na wasanii wenyewe.
Wasanii hao wa miondoko ya Hip Hop wameelezea kuwa kutengana kwao haimaanishi ndio mwisho wao katika kufanya muziki, bali kila mmoja ameona ni bora ajishughulishe na project zake binafsi.
Imeelezwa kuwa taio Tripper, K'cous na Miss Karun wanatarajia kuondoka nchini kwa ajili ya kujiendeleza zaidi na masomo wakati Shappaman aatabakia nchini Kenya na kuendelea kufocus na taalu

DOWNLOAD LORD EYEZ FT DAMIAN-MAPITO

YA KUKUMBUKWA MIAKA 29 KIFO CHA SOKOINE

Ilikuwa Jumatano ya Aprili 12, 1984 saa 11:30 jioni, siku ambayo Dar es Salaam ilinyesha mvua kutwa nzima. Wakati kipindi cha salaam cha Jioni Njema cha Redio Tanzania (RTD) wakati huo kikiwa hewani, mara matangazo yake yanakatishwa ghafla na wimbo wa taifa unapigwa.
Mara inasikika sauti iliyozoeleka ya Rais Nyerere wakati huo ikisema: “Ndugu wananchi, leo majira ya saa 10 jioni, ndugu yetu, kijana wetu na mwenzetu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine wakati akitoka Dodoma kuja Dar es Salaam, gari yake imepata ajali, amefariki dunia.”
Takribani miaka 29 imepita tangu kufariki kwa, Edward Moringe Sokoine, aliyepata kuwa waziri mkuu wa Tanzania katika vipindi viwili tofauti kabla ya kufariki Aprili 12, 1984.
Sokoine alikufa baada ya kutokea ajali ya gari eneo la Wami-Dakawa, wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea mjini Dodoma alikokuwa akishiriki vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kumbukumbuka kila mwaka
Aprili 12 ya kila mwaka, taifa limekuwa likiadhimisha kumbukumbu ya kiongozi huyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kuendesha makongamano, midahalo, mabonanza, ibada, riadha na upandaji mlima Kilimanjaro.
Katika utawala wa hayati baba wa taifa na rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika eneo la Wami  Sokoine kulijengwa nyumba moja na banda moja linalotumika kama jukwaa lakini kwa sasa majengo hayo yamechakaa, anasema msimamizi wa eneo hilo, Hamis Said Mpandachuri.
Mwananchi ilifika katika eneo hilo na kukuta mnara wa picha ya Sokoine ukiwa umepakwa rangi mpya za manjano, kijani, blue na nyeusi huku chini ya picha yake kukiwa na maneno “Alimtumikia Mungu kwa kuwatumikia watu, sauti ya watu ni sauti ya Mungu”.
Mbali ya mnara huo na majengo yaliyojengwa katika utawala wa serikali ya kwanza, pia liko jengo jipya na la kisasa ambalo linaendelea kujengwa nyuma ya majengo ya zamani. Kwa mujibu wa uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero, jengo hilo ni kwa ajili ya shule ya sekondari ya Sokoine (Sokoine memorial high school), inajengwa kama sehemu ya jitihada za wilaya hiyo za kumuenzi Sokoine.
Mbali na jitihada za halmashauri hiyo, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ambacho pia kimebeba jina lake kimekuwa katika mikakati ya kuhakikisha kuwa kinamuenzi kiongozi huyo kwa kila hali. Kassim Msagati ni ofisa mawasiliano wa chuo hicho,  anasema hayati, Edward Moringe Sokoine, alikuwa muhimili muhimu wa kuanzishwa wa chuo kikuu hicho cha kilimo ambacho ni chuo kikuu pekee cha kilimo cha Serikali nchini.
Aprili 12, 1984 bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo hayati Sokoine alishiriki lilipitisha sheria namba 6 ya mwaka 1984 ya kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kilimo Morogoro. Hapo kabla chuo hicho kilikuwa ni kitivo cha kilimo cha kilimo na misitu cha chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Msagati, sheria hiyo iliyopitishwa na bunge ilikiidhinisha kitivo cha kilimo cha chuo kikuu cha Dar es salaam kilichokuwa Morogoro kuwa chuo kikuu na kutaka kiitwe chuo kikuu cha kilimo Morogoro.
Lakini chuo hicho kililazimika kubadilishwa jina hata kabla ya jina la awali kuanza kutumika na kuitwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA). Hii ilitokana na kifo cha kiongozi huyo, muda mfupi baada ya chuo hicho kuidhinishwa rasmi kwa sheria hiyo ambapo utekelezaji wake ulipaswa kuanza mwezi Julai, 1984, ndipo serikali ikakubali kiitwe Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo.

BARAZA LA KIBAKI LAFUTWA

Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza kumalizika kwa muda wa Serikali ya muungano iliyopita, hivyo kufungua njia ya uteuzi wa Baraza Jipya la Mawaziri litakaloongoza Serikali yake.
Hatua ya Kenyatta inamaanisha kumaliza zama za utawalka wa Rais Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake, baada ya uchaguzi uliofanyika Machi 4 na kumpa ushindi Kenyatta pamoja na mgombea mwenza wake, William Ruto.
“Kwa mujibu wa Katiba Mpya ya Kenya iliyopitishwa mwkaa 2010, Serikali iliyokuwa ikiongozwa na Rais Mwai Kibaki ilimaliza muda wake usiku wa Aprili 9,” alieleza Kenyatta katika taarifa yake iliyosambazwa na Ikulu ya mjini Nairobi.
Agizo hilo linawahusu wanasiasa waliokuwa katika nafasi za kuteuliwa hasa mawaziri na manaibu wao, ambapo ilieleza kwamba kwa sasa makatibu wakuu wa Wizara ndio watakaoendesha shughuli zote hadi mawaziri wapya watakapotangazwa rasmi.
Taarifa hiyo ilitolewa katika siku ya kwanza ya Kenyatta ofisini akiwa mkuu wa nchi, pamoja na msaidizi wake, Ruto, ambapo walikuwa wakipokea taarifa kutoka kwa wakuu wa usalama, maofisa wa Serikali, mwelekeo wa maandalizi ya bajeti na kupitia kwa mara ya mwisho namna ya muundo wa serikali wanayoihitaji.

MKAPA ,KOFFI ANNANI WAINGIA MTINI














 





Maoni ya Annan yaliibua mjadala mkubwa kutoka kwa Wakenya wengine wakamchukia
Nairobi. Kundi muhimu ambalo lilisaidia kwa karibu kuunda Serikali ya Kenya ambalo lilikuwa likiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan halikuweza kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.
Taarifa kutoka Kenya zilisema kwamba Kofi Annan ambaye aliongoza kuundwa kwa Serikali ya Muungano baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2007 hakuweza kuonekana katika sherehe hizo.
Pia waliokosekana ni wanachama wa kundi la Dk Annan ambao ni pamoja na Graca Machel na Benjamin Mkapa. Kundi hilo ndilo lilisaidia kuunda Serikali hiyo.
Lakini muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu,  Annan alitaka uchaguzi nchini ufanyike kwa amani.
Mwaka jana ,  Annan aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alizua malumbano alipowahimiza Wakenya wasiwachague wanasiasa walioshtakiwa na Mahakama ya Kimataifa Kuhusu Uhalifu (ICC).
Ingawaje hakuwataja Rais Kenyatta na Naibu wake William Ruto, wanaokabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama hiyo iliyopo The Hague, Uholanzi,  Annan aliliambia shirika la BBC kuwa kuwachagua viongozi wa aina hiyo kutaathiri uhusiano wa Kenya na jamii ya kimataifa.
Maoni yake yaliibua majibu kutoka kwa wafuasi wa chama cha Rais Kenyatta cha The National Alliance (TNA) na wa United Republican Party (URP) cha  Ruto.