Kwa
muda kumekuwa na stories kibao tofauti tofauti zisizo nzuri kuhusiana
na G.Unit Crew, 50 cent mwenyewe amekubali washkaji kweli hawaongei kama
vile kwa sasa. Akipiga stories na MTV Tony Yayo alizungumza juu ya
hilo. Alisema kipindi wakiwa na mkwanja mambo yalikuwa mabaya sana
mkwanja ndo chanzo cha ushetani wote, lakini kipindi tukiwa hatuna
mkwanja mambo yalikuwa fresh tu, Alisema hivyo akipiga stories na MTV.
Siku
nyingine tena, Drama nyingine tena, lakini sio msanii mwingine, msanii
ni Yule Yule mkali ambae anadrama kibao, juzi wakaleteana noma na Frank
Ocean. Sasa basi unakumbuka siku za nyuma Chriss Brown alidelete twitter
account yake? na baada ya siku mbili au moja baadae akairudisha ilikuwa
ni baada ya kujibishana sana na mtu kwenye twitter. Drama za Chriss
Brown muda mwingine huwa zinasababishwa na yeye mwenyewe au saa nyingine
unakuta hausiki. Sasa basi Mshikaji Chriss Brown kufuatia drama yake na
Frank Ocean juzi kati ameamua kufuta instagram yake na alikuwa akiandika
meseji za drama ile mbaya na kutangaza kuondoka kwake yani kufuta
instagram yake, Swali ni kwamba, Je Chriss Brown atarudi tena instagram
kama alivyofanya kwenye twitter au ndo ntoleeeee? Turn Up Lol!