Monday, February 04, 2013
XAVI HERNÁNDEZ NJE KWA SIKU 15
MADUKA YATEKETEA KWA MOTO MWENGE
Licha ya Moto huo kuonesha kuwa na madhara zaidi, vikosi vya zimamoto vikishirikiana na vile vya Kampuni binafsi za Ulinzi vilifanikiwa kuuzima moto huo na kupunguza hatari ya kuhamia kwenye maduka mengine ambayo yamekaribiana.
Akizungumzia
tukio, Mkuu wa Ulinzi Shirikishi Kituo cha Mabasi Mwenge KESSY MLUGURU
amesema, waligundua kutokea kwa moto huo katika moja ya duka majira ya
saa tatu asubuhi na kuanza juhudi za kuuzima kwa maji yakiyo kwenye
tenki ambapo Mkuu wa Kituo cha Polisi Mabatini Kijitonyama anathibitisha
kutokea kwa moto huo.
Mmoja ya Wamiliki wa maduka ya vipodozi ambayo yameteketea MAPINDUZI WILSON amesema, moto huo umetokea kutokana na hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye moja ya waya zinazoingia kwenye maduka hayo.
Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, Meja KURWA NZELEKELA amesema kikosi chake kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu ya barabarani na usalama wanapokuwa kazini.
Tukio hili linafuatiwa na lile lililotokea jana kwenye Jengo la PPF TOWER lililopo Makutano ya Mtaa wa Ohio na Garden kunusurika kuteketea kwa moto baada ya moja ya ghorofa zake kushika moto ambao pia ulidhibitiwa na vikosi hivyo vya zima moto.

TUME YA KUKUSANYA NA KURATIBU MAONI YA KATIBA YAMALIZA HATUA ZA MSINGI
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu JOSEPH WARIOBA amesema kuwa uchambuzi huo unatarajiwa kufanywa na mabaraza maalum ya Katiba kuanzia June Mwaka huu, na kuongeza kuwa mabaraza hayo yatapatikana kupitia mapendekezo maalum kutoka kwa wajumbe wa Tume hiyo.
Akizungumzia uteuzi wa mabaraza hayo JAJI WAROBA amesema, tume hiyo imejipanga kuhakikisha watu watakaopatikana kuunda mabaraza hayo wanakuwa makini, na ambao watasimamia zoezi hilo haraka na kwa umakini zaidi ili kupata katiba itakayokuwa na tija kwa Watanzania.
LEO KATIKA ITV HABARI
Subscribe to:
Posts (Atom)