Madai
ya kundi moja la wapiganaji wa kiisilamu nchini Nigeria, kuwa limewaua
mateka 7 wa kigeni waliowateka mwezi wa februari huenda ni ya kweli.Mateka
hao kutoka nchini Italy, Uingereza, Ugiriki, na Lebanon, walitekwa
katika eneo la jengo katika jimbo la Bauchi Kaskazini .Katika taarifa kupitia mitandao, siku ya Jumamosi,kundi la wapiganaji la Ansaru lilidai kuwaua mateka hao.Ansaru linashukiwa kuwa kundi lenye kuendesha harakati sawa na za Boko Haram.Jumapili,
waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague, alisema kuwa
mfanyakazi wa mjengo aliyetajwa kama Brendan Vaughan, huenda aliuawa na
watu waliokuwa wamemteka, pamoja na wenzake 6.Serikali
ya Italia iliwasilisha taarifa sawa na hiyo wakati wizara ya mambo ya
nje ya Ugiriki ikisema , kuwa taarifa waliyonayo inaonyesha kuwa raia
wake wameuawa.
Mchezaji
wa Barcelona Andres Iniesta anasema timu yake leo inatakiwa iitumie
siku hii ya Jumanne kama ndo fainali katika Champion league ikiwa ni
mzunguko wa mwisho wa 16 wakiwa nyumbani wakiwakabili AC Milan.
Barcelona inatakiwa watengeneze kwa sababu walifungwa 2 – 0 “Itakuwa
ngumu lakini sio kwamba haiwezekani” “Tunatakiwa tucheze kama vile ni
fainali hivyo ndivyo invyotakiwa tuweke akili zetu kuanzia dakika ya
kwanza mpaka ya mwisho” Alisema Iniesta. Barcelona haijapoteza ikiwa
ndani ya Nou Camp toka Octoba 20, 2009, Timu hiyo kutoka Uispania
iliifunga AC Miln kwenye msimu wa mwisho robo fainali na mwaka 2005 – 6
kwenye nusu finali.