MTANGAZAJI wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida,’ hivi
karibuni alinaswa akiwa amevalia kiatu ambacho kina silaha.
Kiatu hicho ambacho ni moja ya fasheni zilizoingia, kina misumari pembeni kiasi kwamba akikurushia teke, ni lazima kikutoboe.
Baadhi ya watu waliokiona kiatu hicho walisema kuwa, licha ya kwamba ni fasheni lakini atakayekivaa lazima watu wamgwaye.
“Sasa
hiki ni kiatu au silaha? Ukikivaa kwenye msongamano wa watu si
utajeruhi, mh! Hizi fasheni za sasa mbona balaa,” alisema Zuhura wa
Kinondoni.