Akizungumza na na safu hii leo jijini Dar, Herieth
Chumila ambaye pia ni msanii, alisema alipokea taarifa za kuumwa kwa
Matumaini kutoka kwa mtoto wake aishiye nchini humo na kumwomba msaada
wa haraka kwa kuwa msanii huyo yupo katika hali mbaya.
Herieth alisema kwa sasa msanii huyo hawezi hata kutembea na mahitaji muhimu ya kibinadamu anayamalizia kitandani.
“Nilipata
bahati ya kuongea na Matumaini ingawa kwa shida sana, aliwaomba
Watanzania tumsaidie ili arudi nyumbani. Alisema ni bora aje kufia huku
kuliko nchi za watu,” alisema Herieth.
Akaongeza: “Kwa yule ambaye
ataguswa kumchangia awasiliane na mimi kwa ajili ya mchango ambao
utamfikia Matumaini kule Msumbiji.”
No comments:
Post a Comment