Friday, April 12, 2013
CAMP MULLA WATETE BAADA YA KUTENGANA
Uvumi umezidi kutanda kuhusu kutengana kwa wasanii
wanaoliwakilisha kundi maarufu la Camp Mulla la nchini Kenya na ukweli wa jambo
hilo limewekwa wazi na wasanii wenyewe.
Wasanii hao wa miondoko ya Hip Hop wameelezea kuwa
kutengana kwao haimaanishi ndio mwisho wao katika kufanya muziki, bali kila
mmoja ameona ni bora ajishughulishe na project zake binafsi.
YA KUKUMBUKWA MIAKA 29 KIFO CHA SOKOINE
Mara inasikika sauti iliyozoeleka ya Rais Nyerere
wakati huo ikisema: “Ndugu wananchi, leo majira ya saa 10 jioni, ndugu
yetu, kijana wetu na mwenzetu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Edward Moringe Sokoine wakati akitoka Dodoma kuja Dar es
Salaam, gari yake imepata ajali, amefariki dunia.”
Takribani miaka 29 imepita tangu kufariki kwa,
Edward Moringe Sokoine, aliyepata kuwa waziri mkuu wa Tanzania katika
vipindi viwili tofauti kabla ya kufariki Aprili 12, 1984.
Sokoine alikufa baada ya kutokea ajali ya gari
eneo la Wami-Dakawa, wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro akiwa njiani
kurejea Dar es Salaam akitokea mjini Dodoma alikokuwa akishiriki vikao
vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kumbukumbuka kila mwaka
Aprili 12 ya kila mwaka, taifa limekuwa likiadhimisha kumbukumbu ya kiongozi huyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kuendesha makongamano, midahalo, mabonanza, ibada, riadha na upandaji mlima Kilimanjaro.
Aprili 12 ya kila mwaka, taifa limekuwa likiadhimisha kumbukumbu ya kiongozi huyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kuendesha makongamano, midahalo, mabonanza, ibada, riadha na upandaji mlima Kilimanjaro.
Katika utawala wa hayati baba wa taifa na rais wa
kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwalimu Julius Kambarage
Nyerere, katika eneo la Wami Sokoine kulijengwa nyumba moja na banda
moja linalotumika kama jukwaa lakini kwa sasa majengo hayo yamechakaa,
anasema msimamizi wa eneo hilo, Hamis Said Mpandachuri.
Mwananchi ilifika katika eneo hilo na kukuta mnara
wa picha ya Sokoine ukiwa umepakwa rangi mpya za manjano, kijani, blue
na nyeusi huku chini ya picha yake kukiwa na maneno “Alimtumikia Mungu
kwa kuwatumikia watu, sauti ya watu ni sauti ya Mungu”.
Mbali ya mnara huo na majengo yaliyojengwa katika
utawala wa serikali ya kwanza, pia liko jengo jipya na la kisasa ambalo
linaendelea kujengwa nyuma ya majengo ya zamani. Kwa mujibu wa uongozi
wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero, jengo hilo ni kwa ajili ya shule ya
sekondari ya Sokoine (Sokoine memorial high school), inajengwa kama
sehemu ya jitihada za wilaya hiyo za kumuenzi Sokoine.
Mbali na jitihada za halmashauri hiyo, Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ambacho pia kimebeba jina lake kimekuwa
katika mikakati ya kuhakikisha kuwa kinamuenzi kiongozi huyo kwa kila
hali. Kassim Msagati ni ofisa mawasiliano wa chuo hicho, anasema
hayati, Edward Moringe Sokoine, alikuwa muhimili muhimu wa kuanzishwa wa
chuo kikuu hicho cha kilimo ambacho ni chuo kikuu pekee cha kilimo cha
Serikali nchini.
Aprili 12, 1984 bunge la jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambalo hayati Sokoine alishiriki lilipitisha sheria namba 6 ya
mwaka 1984 ya kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kilimo Morogoro. Hapo kabla
chuo hicho kilikuwa ni kitivo cha kilimo cha kilimo na misitu cha chuo
kikuu cha Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Msagati, sheria hiyo iliyopitishwa
na bunge ilikiidhinisha kitivo cha kilimo cha chuo kikuu cha Dar es
salaam kilichokuwa Morogoro kuwa chuo kikuu na kutaka kiitwe chuo kikuu
cha kilimo Morogoro.
Lakini chuo hicho kililazimika kubadilishwa jina
hata kabla ya jina la awali kuanza kutumika na kuitwa Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo (SUA). Hii ilitokana na kifo cha kiongozi huyo, muda
mfupi baada ya chuo hicho kuidhinishwa rasmi kwa sheria hiyo ambapo
utekelezaji wake ulipaswa kuanza mwezi Julai, 1984, ndipo serikali
ikakubali kiitwe Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo.
BARAZA LA KIBAKI LAFUTWA
Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza kumalizika kwa
muda wa Serikali ya muungano iliyopita, hivyo kufungua njia ya uteuzi wa
Baraza Jipya la Mawaziri litakaloongoza Serikali yake.
Hatua ya Kenyatta inamaanisha kumaliza zama za
utawalka wa Rais Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake, baada ya uchaguzi
uliofanyika Machi 4 na kumpa ushindi Kenyatta pamoja na mgombea mwenza
wake, William Ruto.
“Kwa mujibu wa Katiba Mpya ya Kenya iliyopitishwa
mwkaa 2010, Serikali iliyokuwa ikiongozwa na Rais Mwai Kibaki ilimaliza
muda wake usiku wa Aprili 9,” alieleza Kenyatta katika taarifa yake
iliyosambazwa na Ikulu ya mjini Nairobi.
Agizo hilo linawahusu wanasiasa waliokuwa katika
nafasi za kuteuliwa hasa mawaziri na manaibu wao, ambapo ilieleza kwamba
kwa sasa makatibu wakuu wa Wizara ndio watakaoendesha shughuli zote
hadi mawaziri wapya watakapotangazwa rasmi.
Taarifa hiyo ilitolewa katika siku ya kwanza ya
Kenyatta ofisini akiwa mkuu wa nchi, pamoja na msaidizi wake, Ruto,
ambapo walikuwa wakipokea taarifa kutoka kwa wakuu wa usalama, maofisa
wa Serikali, mwelekeo wa maandalizi ya bajeti na kupitia kwa mara ya
mwisho namna ya muundo wa serikali wanayoihitaji.
MKAPA ,KOFFI ANNANI WAINGIA MTINI
Maoni ya Annan yaliibua mjadala mkubwa kutoka kwa Wakenya wengine wakamchukia
Nairobi. Kundi muhimu ambalo
lilisaidia kwa karibu kuunda Serikali ya Kenya ambalo lilikuwa
likiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan
halikuweza kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.
Taarifa kutoka Kenya zilisema kwamba Kofi Annan
ambaye aliongoza kuundwa kwa Serikali ya Muungano baada ya Uchaguzi Mkuu
wa 2007 hakuweza kuonekana katika sherehe hizo.
Pia waliokosekana ni wanachama wa kundi la Dk Annan ambao ni pamoja na Graca Machel na Benjamin Mkapa. Kundi hilo ndilo lilisaidia kuunda Serikali hiyo.
Pia waliokosekana ni wanachama wa kundi la Dk Annan ambao ni pamoja na Graca Machel na Benjamin Mkapa. Kundi hilo ndilo lilisaidia kuunda Serikali hiyo.
Lakini muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu, Annan alitaka uchaguzi nchini ufanyike kwa amani.
Mwaka jana , Annan aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa alizua malumbano alipowahimiza Wakenya wasiwachague
wanasiasa walioshtakiwa na Mahakama ya Kimataifa Kuhusu Uhalifu (ICC).
Ingawaje hakuwataja Rais Kenyatta na Naibu wake
William Ruto, wanaokabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu
katika mahakama hiyo iliyopo The Hague, Uholanzi, Annan aliliambia
shirika la BBC kuwa kuwachagua viongozi wa aina hiyo kutaathiri uhusiano
wa Kenya na jamii ya kimataifa.
Maoni yake yaliibua majibu kutoka kwa wafuasi wa
chama cha Rais Kenyatta cha The National Alliance (TNA) na wa United
Republican Party (URP) cha Ruto.
Subscribe to:
Posts (Atom)