XAVI HERNÁNDEZ NJE KWA SIKU 15
Baada
ya kufanyiwa majaribio asubuhi ya leo Xavi Hernandez imegundulika
kwamba atakuwa nje kwa takribani siku 15 na atakosa mechi mbili zijazo
kati ya Getafe na Granada, Ingawa kupona kwake kunaenda kama
ilivyopangwa, Xavi atarudi uwanjani wakati michezo ya Champion League
wakicheza na Milan mechi itakayochezwa tarehe 20 mwezi 20. Xavi pia
atakosa pia mechi kati ya kirafiki dhidi ya Uruguay Jumatano. Xavi
amecheza mara 33 msimu huu na amefunga magoli 6, Xavi alicheza karibia
mechi yote Jumapili pale Mestalla na alitoka na kubadilishana na Thiago
katika muda wa nyongeza.
No comments:
Post a Comment