Advertise here

Friday, February 01, 2013

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko kuu Mwanza akutwa na jeneza..

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko kuu jijini Mwanza Bw. Hamad Nchola anadaiwa kukutwa na jeneza ambalo hata hivyo halikuwa na maiti ndani yake, likiwa katikati ya magunia ya viazi mviringo na hivyo kusababisha umati wa watu kufurika ndani ya soko hilo huku baadhi yao wakilihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

Waziri mkuu awasilisha taarifa kuhusu mgogoro wa gesi Mtwara.

Kidis ft DNA,Ameleena,Wyre- KAMUA LEO 2013

HUYU NDIO MWIMBAJI MKENYA AMBAE MAMA YAKE NI MTANZANIA, KAVUNJA REKODI KUSHIRIKI AMERICAN IDOL, TAZAMA NICKI MINAJ NA MARIA CAREY WAKIMUONGELEA

Sanni M'mairura Sings *Whos Loving You* American Idol Auditions

Anaitwa Sanni M’mairura.
Sio kazi rahisi kuingia kwenye moja ya mashindano MAKUBWA DUNIANI ya AMERICAN IDOL, sio kazi ndogo hata kidogo, SANNI M’MAIRURA ndio Mtanzania wa kwanza mimi kusikia kaingia kwenye haya mashindano ambayo majaji wake wa sasa hivi ni pamoja na mastaa wa muziki duniani Maria Carey na rapper Nicki Minaj, tazama hiyo video hapo juu

DIAMOND AFUNGUKA: WANAOSEMA KASHUKA KISANII, HUU NDIO MWISHO WAKE

Diamond Platnums.
Kwa kipindi kirefu kidogo toka mwaka 2012 kumekua na taarifa mbalimbali zinazopita kwenye magazeti, blogs na midomoni mwa watu kadhaa kwamba staa wa muziki wa bongofleva anaetajwa kulipwa pesa kubwa kwenye kufanya show Tanzania Diamond Platnums ameshuka kiwango, yani mwisho wake kwenye muziki umefika.

Baada ya hizo taarifa nimekua nikijaribu kufanya interview na Diamond lakini hakupenda kuliongelea hilo kwa wakati huo.

Diamond amebadili huo msimamo na kuamua kufunguka rasmi kuhusu yote yanayosemwa kwamba kashuka kiwango.

Namnukuu akisema “unapofanya vizuri hakuna anaependa, kama Maisha Club wasanii wengi huwa wanafanya show lakini nikifanya mimi ndio panatapika hata club nyingi hata nilivyofanya show Dar Live uliona watu kutaka kutia virusi, kutaka kutengenezea mazingira”
“Mashabiki ndio wanatakiwa kusema flani labda sasa hivi ameshuka lakini mashabiki hao ndio hao kila siku wanazidi kununua kazi zangu, wanazidi kuomba nyimbo zangu kwenye redio.. kiukweli nyimbo zangu ndio zinaombwa sana kwenye radio, katika show zangu wanajaa sana” – Diamond

Kwenye sentensi nyingine Diamond amesema “kuna gazeti likaandika Diamond sijui ndio mwaka wake wa mwisho, Diamond sijui ameshuka kiwango… utaweza vipi kuandika vitu kama hivyo? mi ndio msanii ambae nalipwa pesa nyingi kuliko msanii mwingine yoyote Tanzania, vita za kibiashara kokote zipo mimi ndio maana hazinishtui kila siku ndio maana nazidi kuachia ngoma tu kuwakata vilimi vilimi, wanatakiwa wajue kabisa kwamba mimi nimeaga nyumbani… licha ya kuaga mi nafanya muziki kama kazi kwa njaa kabisa, kwa hiyo mwenyezi Mungu alienipandisha na mashabiki zangu ndio wanaweza wakataka kunishusha”

Wednesday, January 30, 2013

WAKATI G.UNIT HAWANA MKWANJA MAMBO YALIKUWA AAH FRESH!!

Kwa muda kumekuwa na stories kibao tofauti tofauti zisizo nzuri kuhusiana na G.Unit Crew, 50 cent mwenyewe amekubali washkaji kweli hawaongei kama vile kwa sasa. Akipiga stories na MTV Tony Yayo alizungumza juu ya hilo. Alisema kipindi wakiwa na mkwanja mambo yalikuwa mabaya sana mkwanja ndo chanzo cha ushetani wote, lakini kipindi tukiwa hatuna mkwanja mambo yalikuwa fresh tu, Alisema hivyo akipiga stories na MTV.

CHRISS BROWN NDANI YA DRAMA NYINGINE

Siku nyingine tena, Drama nyingine tena, lakini sio msanii mwingine, msanii ni Yule Yule mkali ambae anadrama kibao, juzi wakaleteana noma na Frank Ocean. Sasa basi unakumbuka siku za nyuma Chriss Brown alidelete twitter account yake? na baada ya siku mbili au moja baadae akairudisha ilikuwa ni baada ya kujibishana sana na mtu kwenye twitter.  Drama za Chriss Brown muda mwingine huwa zinasababishwa na yeye mwenyewe au saa nyingine unakuta hausiki. Sasa basi Mshikaji Chriss Brown kufuatia drama yake na Frank Ocean juzi kati ameamua kufuta instagram yake na alikuwa akiandika meseji za drama ile mbaya na kutangaza kuondoka kwake yani kufuta instagram yake, Swali ni kwamba, Je Chriss Brown atarudi tena instagram kama alivyofanya kwenye twitter au ndo ntoleeeee? Turn Up Lol!