KUNA UWEZEKANO KUND LA HIP HOP LA G UNIT KURUDI TENA
Mkali
50 cent amesema anaweza kurudi studio kufanya kazi na original members
wa G.Unit Lloyd Banks na Tony Yayo. Kwa kipindi cha miaka miwili 50 cent
alirudia kwenye mahojiano kwamba yeye na washkaji Lloyd Banks na Tony
Yayo wamekuwa mbali. Tumaini la G.Unit kurudi lipo. 50 cent alisema
kwenye Billboard.biz kwamba walikuwa na utofauti lakini wamekuwa
wanafanya mipango warudi na kuendelea kufanya kazi. Wakati wa mahojiano
50 cent aliongelea album yake inayokuja ya “Street King Immortal”
itaingia dukani Februari 26. Album hiyo ambayo imekutana na mambo kibao
ambayo yameifanya album hiyo ichelewe itakuwa ya kwanza toka 2009 alipoingia kwenye tafrani na Interscope kwenye mikataba. 50 cent amesema Project hiyo itakuwa na ngoma 13 – 14 na amerekodi ngoma 70 kwa ajili ya album hiyo.
No comments:
Post a Comment