DMX TENA KIZIMBANI
Mkali
kutoka nchini Marekani ambaye ameshasumbua sana kwenye game la Hip hop
duniani muite DMX hit maker wa Ruff Ryder Anthem, Leo asubuhi alikamatwa
kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na leseni huko kusini mwa
Carolina. Emcee huyo alifungwa pingu na kupelekwa kizuizini huko
Spartanburg Detention Center mida ya asubuhi saa 2 leo, baada ya askari
kumuona DMX akiendesha 1978 Buick (sweet) ndipo alipomwambia asimame na
kumkuta hana leseni. DMX aliongea na FOX station baada ya kuondoka
Polisi Alisema “ Sikuwa na leseni wakanifunga pingu wakanipeleka polisi
nimelipa mkwanja “ nimepoteza saa 5 pale hata hakuna cha maana” alisema.
Pia kwenye gari hilo alikuwepo mtoto wake wa kike mwenye umri wa miezi 5
tu.
No comments:
Post a Comment