Sunday, January 27, 2013
TAZAMAJUSTIN TIMBERLAKE FT JAY Z Suit & Tie (Official Lyric Video)
Justin Timberlake akimkingia muamvuli Jay Z wakati wa kutengeneza video ya "Suit & Tie".
Timberlake amefunguka kuwa album yake mpya ya 20/20 Experience itatoka mwezi March 19
Saturday, January 26, 2013
OMMY DIMPOZ NA VANESSA MDEE KUANZA KUSHOOT ME & U
Ommy
Dimpoz na Vanessa Mdee wakisindikizwa na AY, jana wamewasili salama
jijini Nairobi Kenya ambako wameenda kushoot video ya Me and You.Video hiyo inafanywa na kampuni ya Ogopa Dj’s ambayo hivi karibuni ilishoot video ya Diamond, Kesho. Me and You ni single ya tatu ya Ommy yenye mafanikio makubwa.
MSANII MATUMAINI YU MAUTUTI MSUMBIJI
Akizungumza na na safu hii leo jijini Dar, Herieth
Chumila ambaye pia ni msanii, alisema alipokea taarifa za kuumwa kwa
Matumaini kutoka kwa mtoto wake aishiye nchini humo na kumwomba msaada
wa haraka kwa kuwa msanii huyo yupo katika hali mbaya.
Herieth alisema kwa sasa msanii huyo hawezi hata kutembea na mahitaji muhimu ya kibinadamu anayamalizia kitandani.
“Nilipata
bahati ya kuongea na Matumaini ingawa kwa shida sana, aliwaomba
Watanzania tumsaidie ili arudi nyumbani. Alisema ni bora aje kufia huku
kuliko nchi za watu,” alisema Herieth.
Akaongeza: “Kwa yule ambaye
ataguswa kumchangia awasiliane na mimi kwa ajili ya mchango ambao
utamfikia Matumaini kule Msumbiji.”
MSANII WA BONGO MATATANI KWA VAA VIATU VYENYE SIRAHA
MTANGAZAJI wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida,’ hivi
karibuni alinaswa akiwa amevalia kiatu ambacho kina silaha.
Kiatu hicho ambacho ni moja ya fasheni zilizoingia, kina misumari pembeni kiasi kwamba akikurushia teke, ni lazima kikutoboe.
Baadhi ya watu waliokiona kiatu hicho walisema kuwa, licha ya kwamba ni fasheni lakini atakayekivaa lazima watu wamgwaye.
“Sasa hiki ni kiatu au silaha? Ukikivaa kwenye msongamano wa watu si utajeruhi, mh! Hizi fasheni za sasa mbona balaa,” alisema Zuhura wa Kinondoni.

Subscribe to:
Posts (Atom)