Advertise here

Saturday, April 20, 2013

KAJALA ATOA YA MOYONI


Kajala ametoka kukumbana na kashikashi katika maisha yake hivi karibuni, baada ya kusota jela takriban mwaka mmoja kutokana na kesi ya kutakatisha fedha iliyomwandama yeye na mumewe ambaye yuko jela.

Akizungumza katika kipindi cha ‘Take One’ kinachorushwa kila Jumanne na Clouds Tv, Kajala alisema alipokuwa jela alimkumbuka mama yake kwa mambo aliyokuwa akimwambia na kuanza kujuta kutokana na mateso aliyokutana nayo huko.
 
           “Mimi nilianza kumkumbuka sana mama yangu alivyokuwa akiniusia kutulia, ila mimi natoroka nyumbani nakwenda ninakotaka na kumuacha katika huzuni, ila nilipokaa jela niliona nini umuhimu wa mama, namuomba anisamehe sikujua nilitendalo,” alisema Kajala
 
Aidha, Kajala alisema katika familia yao, mama yake alikuwa ni mkali kuzidi baba yake, ambaye kila kitu walichotaka kufanya aliwaruhusu, ikiwa ni pamoja na kwenda katika majumba ya muziki, lakini mama yao alikataa na kudai sasa anatambua umuhimu wake.

           Aliwashukuru wote ambao walikuwa naye bega kwa bega hadi kufanikisha kutoka jela, huku shukrani za pekee akizimwaga kwa msanii mwenzake Wema Sepetu ambaye alimnusuru kufungwa jela miaka saba kwa kumlipia faini ya sh milioni 13.

No comments: