Advertise here

Wednesday, February 13, 2013

DMX TENA KIZIMBANI

Mkali kutoka nchini Marekani ambaye ameshasumbua sana kwenye game la Hip hop duniani muite DMX hit maker wa Ruff Ryder Anthem, Leo asubuhi alikamatwa kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na leseni huko kusini mwa Carolina. Emcee huyo alifungwa pingu na kupelekwa kizuizini huko Spartanburg Detention Center mida ya asubuhi saa 2 leo, baada ya askari kumuona DMX akiendesha 1978 Buick (sweet) ndipo alipomwambia asimame na kumkuta hana leseni. DMX aliongea na FOX station baada ya kuondoka Polisi Alisema “ Sikuwa na leseni wakanifunga pingu wakanipeleka polisi nimelipa mkwanja “ nimepoteza saa 5 pale hata hakuna cha maana” alisema. Pia kwenye gari hilo alikuwepo mtoto wake wa kike mwenye umri wa miezi 5 tu.

AMUUNGUZA MKEWE USON KWA PASI

MWANAUME mmoja aliyemuunguza mkewe usoni kwa kutumia pasi ya umeme mjini Singida, Baltazar Mushi a.k.a Sammayuni (33), amefikishwa mahakamani mjini Singida kujibu shitaka la kujeruhi mkewe, Lucy Msuya(30), mwishoni mwa wiki iliopita.
Mbele ya hakimu Asha Mwetindwa, imedaiwa na mwendesha mashitaka inspekta msaidizi wa polisi Shukurani Magafu kuwa, mshitakiwa amefanya kosa hilo usiku wa februari saba mwaka huu, katika eneo la Ipembe Tarafa ya Mungumaji, mjini Singida.
Hata hivyo hakimu Mwetindwa amesema dhamana ipo wazi kwa mshitakiwa, kwa wadhamini wawili ambao kila mmoja awe na Sh. Milioni tano na shauri hilo litatajwa tena mahakamani hapo februari 25, mwaka huu.

SIKU YA RADIO DUNIANI WATANZANIA WAONEKANA KUIHUSUDU SANA RADIO KULIKO TV KULUIKONI

 
Ikiwa leo ni siku ya REDIO DUNIANI baadhi ya wasikilizaji wa chombo hicho wameelezea mchango mkubwa unaotolewa na redio katika mambo mbali mbali ya kijamii huku wengine wakishauri watayarishaji na watangazaji kujitahidi kutunza maadili ya Kitanzania katika kutoa matangazo yao kwa jamii.
Wakiongea katika sehemu tofauji jijini Dar wasikilizaji hao wamesema kuongezeka kwa vituo vya redio mijini na vijijini kumesaidia kuwaamsha watu wengi kimaendeleo na kuwaomba wamiliki wa vyombo hivyo kusogeza matangazo yao vijijini ili Watanzania walioko huko waweze kuendelea kupata matangazo hayo kutokana na watazamaji wa televisheni kuelekea kushindwa kufatilia matangazo hayo kwa kukosa fedha za kununulia vingamuzi na kutegemea redio

NGOMA YA ROMA YAMKERA SUGU a.k.a MR.2

Msanii wa kwanza kufanya album hapa Bongo na kwa sasa ni mbunge wa Mbeya mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi a.k.a  Mr II na wengi  hupenda kumuita Sugu ameonyesha wazi kukerwa na ambao ameuimba   ROMA katika ngoma yake ya 2030, Sugu  alichodai ROMA ana kurupuka na hajui anachokifanya.

Akizungumza katika kipindi cha TV wiki iliyopita Sugu  amesema kuwa  msanii huyo anapaswa kuijua misingi ya hip hop na pia Sugu  amemuonya na kumtaka  roma awe muangalifu na anachokiandika na kukitowa  kwa jamii  na sio kukurupuka kama mtu aliyestuliwa toka usingizini
Sugu amesema yeye ni mfuasi wa hip hop hivyo ukitaka kuwa mwana hip  hop  lazima uzame ndani sana ili ukiandika kitu uwe na uhakika nacho na  si  kufanya kama Roma anavyofanya.Namtahadharisha bwana mdogo awe  muangalifu  na anachokiandika na si kukurupuka hip hop ina misingi yake  na ni  lazima uzame ndani sana maana hip hop ni maisha na ukweli mtupu,  pia  aelewe hip hop ni sauti ya kumkombowa mnyonge sasa unapoimba mambo  ambayo huna uhakika nayo haipendezi maana utakuwa hujaisaidia jamii   husika alisema sugu.
Katika  wimbo  huo wa 2030 kuna kipande kina sema pesa ndio imemaliza vita   yaRuge na Sugu kitu ambacho kimeonyesha kumkera Sugu na kusema kuwaRoma  anakurupuka na kuandika asichokijua maana kwa mstari huo tu umefanya   niaamini kila achoandika hana anachokijua maana mstari huu unanihusu na  hakuna ukweli juu ya alichokiimba.

  Sugu amemtaka Roma kusikiliza nyimbo walizoimba kaka zake ili   zimuongoze katika sanaa yake amesema asikize nyimbo kama za profesa   jay,afande sele,solo thang atagunduwa kuwa zilikuwa ni harakati za   uhakika mfano mdogo amesema asikilize miss Tanzania ya Solo Thang atajua  anachomaanisha.

 Roma alipotafutwa  kujua amejisikiaje baada ya mheshimiwa kuchukizwa na wimbo wake Roma   alisema Sugu ni kaka yake na anaamini kama kuna baya atamuita na   atamrekebisha.