Advertise here

Wednesday, February 13, 2013

DMX TENA KIZIMBANI

Mkali kutoka nchini Marekani ambaye ameshasumbua sana kwenye game la Hip hop duniani muite DMX hit maker wa Ruff Ryder Anthem, Leo asubuhi alikamatwa kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na leseni huko kusini mwa Carolina. Emcee huyo alifungwa pingu na kupelekwa kizuizini huko Spartanburg Detention Center mida ya asubuhi saa 2 leo, baada ya askari kumuona DMX akiendesha 1978 Buick (sweet) ndipo alipomwambia asimame na kumkuta hana leseni. DMX aliongea na FOX station baada ya kuondoka Polisi Alisema “ Sikuwa na leseni wakanifunga pingu wakanipeleka polisi nimelipa mkwanja “ nimepoteza saa 5 pale hata hakuna cha maana” alisema. Pia kwenye gari hilo alikuwepo mtoto wake wa kike mwenye umri wa miezi 5 tu.

No comments: