Advertise here

Wednesday, February 13, 2013

AMUUNGUZA MKEWE USON KWA PASI

MWANAUME mmoja aliyemuunguza mkewe usoni kwa kutumia pasi ya umeme mjini Singida, Baltazar Mushi a.k.a Sammayuni (33), amefikishwa mahakamani mjini Singida kujibu shitaka la kujeruhi mkewe, Lucy Msuya(30), mwishoni mwa wiki iliopita.
Mbele ya hakimu Asha Mwetindwa, imedaiwa na mwendesha mashitaka inspekta msaidizi wa polisi Shukurani Magafu kuwa, mshitakiwa amefanya kosa hilo usiku wa februari saba mwaka huu, katika eneo la Ipembe Tarafa ya Mungumaji, mjini Singida.
Hata hivyo hakimu Mwetindwa amesema dhamana ipo wazi kwa mshitakiwa, kwa wadhamini wawili ambao kila mmoja awe na Sh. Milioni tano na shauri hilo litatajwa tena mahakamani hapo februari 25, mwaka huu.

No comments: