Advertise here

Thursday, January 10, 2013

KUNA UWEZEKANO KUND LA HIP HOP LA G UNIT KURUDI TENA

Mkali 50 cent amesema anaweza kurudi studio kufanya kazi na original members wa G.Unit Lloyd Banks na Tony Yayo. Kwa kipindi cha miaka miwili 50 cent alirudia kwenye mahojiano kwamba yeye na washkaji Lloyd Banks na Tony Yayo wamekuwa mbali. Tumaini la G.Unit kurudi lipo. 50 cent alisema kwenye Billboard.biz kwamba walikuwa na utofauti lakini wamekuwa wanafanya mipango warudi na kuendelea kufanya kazi. Wakati wa mahojiano 50 cent aliongelea album yake inayokuja ya “Street King Immortal” itaingia dukani Februari 26. Album hiyo ambayo imekutana na mambo kibao ambayo yameifanya album hiyo ichelewe itakuwa ya kwanza toka 2009 alipoingia kwenye tafrani na Interscope kwenye mikataba.
50 cent amesema Project hiyo itakuwa na ngoma 13 – 14 na amerekodi ngoma 70 kwa ajili ya album hiyo.

No comments: