Advertise here

Tuesday, March 12, 2013

MATEKA SABA WAUAWA NIGERIA.

Madai ya kundi moja la wapiganaji wa kiisilamu nchini Nigeria, kuwa limewaua mateka 7 wa kigeni waliowateka mwezi wa februari huenda ni ya kweli.
Mateka hao kutoka nchini Italy, Uingereza, Ugiriki, na Lebanon, walitekwa katika eneo la jengo katika jimbo la Bauchi Kaskazini .
Katika taarifa kupitia mitandao, siku ya Jumamosi,kundi la wapiganaji la Ansaru lilidai kuwaua mateka hao.
Ansaru linashukiwa kuwa kundi lenye kuendesha harakati sawa na za Boko Haram.
Jumapili, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague, alisema kuwa mfanyakazi wa mjengo aliyetajwa kama Brendan Vaughan, huenda aliuawa na watu waliokuwa wamemteka, pamoja na wenzake 6.
Serikali ya Italia iliwasilisha taarifa sawa na hiyo wakati wizara ya mambo ya nje ya Ugiriki ikisema , kuwa taarifa waliyonayo inaonyesha kuwa raia wake wameuawa.

No comments: